English version

Umma wa Wapanda Baiskeli Dar es Salaam

Dar es Salaam

[Utambulisho ] [Mikutano ] [Habari ] [Katiba ] [Kamati ] [Dondoo ] [Ripoti za Miaka ] [Nunua baisikeli ] [Taarifa kwa waandishi wa habari, kipeperushi, bango ] [Matumizi ya baiskeli Dar es Salaam ] [Mawazo yetu ] [Picha ] [Sheria na sera za Serikali za barabara na usafiri ] [Takwimu ] [Orodha ya Madiwani wa Halmashauri na Wabunge wetu ] [Barabara za Dar es Salaam ] [Viunganishi (Links) ] [Wasiliana nasi]

Utambulisho

Jiunga na UWABA!

Mkutano wa UWABA

Rudi juu

Mikutano

Tunakutana ofisini kwetu (Manzese, Sisi kwa Sisi) kila jumamosi saa tisa mchana
Hakuna kiingilio cha kulipa, ni bure kujiunga.
Wapanda baiskeli wote mnakaribisha. Ukisikia mtaarifu mwenzio.

Rudi juu

Habari

Msafara wa Baisikeli: 14 Juni 2015

Msafara wa Baisikeli 12 Mei 2013

Msafara wa Baisikeli wa wiki ya Umoja wa Ulaya ulitokea jumapili tarehe 12 Mei 2013. Wapanda baisikeli zaidi ya 300 walizunguka mjini na mwendo wa pole pole. Wanaume na wanawake, watoto na vijana na wazee, na walemavu wote walionekana. Pia tulikumbuka Tim Manchester, Mmerekani aliyeishi Dar es Salaam alikufa na ajali wakati wa kuendesha baisikeli, pamoja na wapanda baisikeli wengine waliopata ajali. Kauli mbiu ilikuwa "Uraia" na Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Angellah Kairuki.

Msafara wa Baisikeli 10 March 2013

UWABA wakishirikiana na The Sickle-Cell Foundation of Tanzania wamefanikisha msafara wa matembezi ya baisikeli ulioambatana na kikundi cha Jogging kwa nia na lengo la kuchangia utafutaji hela kwa ajili ya kujenga kituo maalumu cha kuhudumia watu wenye tatizo la SICKLE-CELL hapa Tanzania.Imeelezwa kwamba Tanzania ni nchi ya nne Duniani kwa idadi kubwa ya watu wanaosumbuliwa na ugonjwa huu! Msafara huo ulioanzia viwanja vya Mnazi Mmoja uliongozwa na Mgeni rasmi Mbunge wa Ilala Mhe.Mussa Zungu ulijumuisha makundi mbalimbali wakiwemo Watoto,Walemavu,Wanawake,Wazee na Wanaume pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa The National Institute of Medical Research (NIMR) Dr. Mwale Ntuli Malecela na Mwanasayansi Dr Julie Makani ambaye ameshawahi kufanya uchunguzi ulioweza kutambuliwa kimataifa kuhusiana na upungufu wa damu unaoendana na ugonjwa wa SICKLE-CELL. Msafara wa wapanda Baisikeli ulipitia barabara ya Ali Hassan Mwinyi mpaka Biafra na kuelekea Ilala Boma kabla ya kurudi Mnazi Mmoja kulipofanyika hafla iliyoendana na ugawaji zawadi mbalimbali! Mmojawapo wa waandaaji Ndg.Mejor Mbuya alisisitiza umuhimu wa kutumia baiskeli kwa shughuli za kila siku huku pia akiweka mkazo mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka kumi ya kuandaa mikusanyiko ya wapanda Baisikeli!

Msafara wa Baisikeli 2012

Msafara wa Baisikeli

UWABA pamoja na Ubalozi wa Umoja wa Ulaya tuliandaa Msafara wa Baisikeli Dar es Salaam 2012 uliotokea tarehe 13 Mei 2012. Ulikuwa msafara mzuri sana na watu zaidi ya 400 walishiriki, miongoni yao watoto wadogo na wazee. Wageni rasmi walikuwa Mh Dk Seif Seleman Rashidi Naibu Waziri wa Afya na Mbalozi wa Ulaya Filbeto Cerian Sebregondi.

UWABA tunapiga kampeni kuhusu nauli ya maguta kwenye ferry ya Kigamboni

Wanachama na wadereva wa maguta wanaongea na waandishi wa habari

Mwezi wa kwanza mwaka 2012 nauli za ferry ya Kigamboni zilipanda, lakini nauli nyingi zilipanda mara mbili wakati nauli ya maguta ilipanda mara tano, sera ambayo inaongeza umasikini wa wapanda guta wanosafirisha bidhaa kati ya masoko ya Kigamboni na masoko ya mjini. UWABA tulitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu swala hili. Tarehe 7 mwezi wa kwanza wanachama wa UWABA pamoja na wapanda guta waliongea kwenye TV ya Channel 10 na tena kwenye Radio Magic. UWABA pia tumeandika barua kwa Waziri wa Ujenzi (Wizara inayotoa huduma hiyo ya ferry) kuhusu swala hili. Aidha, UWABA tunapiga kampeni ili daraja ya Kigamboni inayopangwa iwe na njia za wapanda baisikeli.

UWABA tunashirikiana na mtafiti wa Denmark

Mwezi Januari mwaka 2012 UWABA tumeshirikiana na Heidi Hoyer kutoka Denmark ambaye anafanya utafiti kuhusu uendeshaji wa baisikeli jijini Dar es Salaam kwa ajili ya masomo yake ya shahada ya master.

Mwanachama wa UWABA anashiriki kwenye Msafara wa Tumaini wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi

Mwezi wa Novemba mwaka 2011 mwanachama wa UWABA Hamadi Bwaja alisafiri na basi kwenye Trans African Climate Change Caravan of Hope mpaka Durban, South Africa, kwa ajili ya mazungumzo ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi. Alibadilisha mawazo na wanaharakati wengine na kuonyesha jinsi baisikeli inaweza kusaidia tatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi. Tunashukuru ForumCC kwa kuwezesha ushirikiano wa UWABA katika msafara huu.

UWABA tunashiriki kwenye sherehe ya mtaa ya Dar es Salaam

Tarehe 26 Novemba 2011, UWABA na Fasta Cycle Messengers walikuwa na mabanda kwenye Dar es Salaam Pedestrian Street Festival. Meya wa Ilala na watu wengine walitembelea mabanda na kupata taarifa kuhusu UWABA.

UWABA tunatoa mada kwenye Mkutano Mkuu wa Barabara Tanzania (Annual Roads Convention 2011)

Mkutano wa Annual Roads Convention wa Shirika la Barabara Tanzania (Tanzania Roads Association TARA) ulitokea tarehe 17-18 Novemba 2011. Kauli mbiu ilikuwa usalama barabarani. UWABA tuliandika paper kwa ajili ya mkutano huo na mwenyekiti wetu Mejah Mbuya alitoa mada.

UWABA tunaleta maoni ya wapanda baisikeli kwenye mkutano wa Afrika ya Usalama Barabarani huko Ethiopia

Tarehe 9 hadi 11 Novemba 2011 mwenyekiti wa UWABA Mejah Mbuya alishiriki kwenye 2nd Africa Road Safety Conference huko Addis Ababa, Ethiopia. Alishiriki kwenye mazungumzo na kuhakikisha usalama wa wapanda baisikeli usisahaulika. Mkutano uliandaliwa na United Nations Economic Commission for Africa, ambao pia waliwezesha UWABA kushiriki. Taarifa zaidi inapatikana kwenye UNECA press release.

Uzinduzi wa Fasta Cycle Messengers

Uzinduzi wa Fasta

Baada ya kukamilika taratibu za usajili, liseni na mafunzo, uzinduzi wa Fasta Cycle Messengers ulitokea tarehe 16 Oktoba 2011 huko Manzese. Mbalozi wa Umoja wa Ulaya Tim Clarke na mke wake Anne Clarke, wadhamini International Centre for Sustainable Cities, washika dau wengine na waandishi wa habari walihudhuria. Tunaomba wote mtumie huduma za Fasta kupeleka vifurushi mlango hadi mlango hapa Dar es Salaam! Fasta sasa wana tovuti wao www.fasta.co.tz.


Polisi wanatembelea banda ya UWABA

UWABA tunashiriki kwenye wiki ya usalama barabarani 2011 huko Kagera

Wanachama wanne wa UWABA walisafiri kwenda Kagera kwa ajili ya wiki ya usalama barabarani tarehe 3 mpaka 8 Oktoba 2011, ambapo walielimisha jamii kuhusu usalama wa baisikeli na walitoa mafunzo ya usalama wa baisikeli kwa wanafunzi wa shule. Tunapenda kuwashukuru Traffic Police kwa ajili ya kutoa udhamini kuwezesha wanachama wetu kushiriki.

UWABA tunarekebisha na kuuza baisikeli kwenye mradi wa Recycle

UWABA sasa tunarekebisha na kuuza baisikeli kutoka kwa Re~Cycle ili kuhamisisha matumizi ya baisikeli na kupata fedha kuendesha miradi wetu. Kama utapenda kununua baisikeli kutoka kwetu tafadhali wasiliana nasi!

Msafara wa Baisikeli wa Moving Planet

Wapanda baisikeli wanafanya alama ya moving planet

Tarehe 24 Septemba 2011 wapanda baisikeli zaidi ya 200 Dar es Salaam walijiunga na maelfu ya wapanda baisikeli nchi mbalimbali duniani kupiga kampeni kuhusu mabadaliko ya tabia ya nchi (climate change) kwenye kampeni ya Moving Planet. Msafara ulikuwa na udhamini kutoka kwa ForumCC.

Mwanachama wa UWABA kwenye finali ya Campaigner Award

Hongera kwa kiongozi wetu Filbert Mbecha ambaye alifika finali ya International Campaigner award ya Sheila McKechnie Foundation, shirika la uingereza wanaosaidia watu wanopiga kampeni. Filbert yupo kwenye website ya SMK.

Msafara wa Baisikeli Mei 2011

Waziri na wageni waalikwa wakiongoza msafara

Msafara wa Baisikeli wa Wiki ya Ulaya tarehe 8 Mei 2011 ulikuwa na wapanda baisikeli zaidi ya 300 wakiendesha pamoja jijini kuonyesha umuhimu wa usalama barabarani kwa wapanda baisikeli. Msafara ulitokea ndani ya Wiki ya Umoja wa Ulaya na ulidhaminiwa na Umoja wa Ulaya Tanzania. Mgeni rasmi Mhe Magufuli Waziri ya Miundombinu alitoa hotuba nzuri kuhusu kuboresha usalama wa wapanda baisikeli. Waziri pamoja na Mbalozi wa EU na wageni waalikwa wengine waliongoza msafara kwa kuendesha baisikeli. Msafara pia ulitokea sambamba na matukio mengine duniani mwezi huu kuzindua "UN Decade of Action on Road Safety 2011-2021".

UWABA tunapokea kontena ya baisikeli kutoka kwa Re-Cycle

Aprili 2011 UWABA tumepokea kontena ya baisikeli kutoka kwa Re-cycle, NGO huko uingereza. UWABA tuna mpango kurekebisha na kuuza baadhi za baisikeli ili kurudisha gharama za kodi, kuanzisha workshop ya fundi baisikeli na kutuwezesha kuingiza nchini kontena zaidi, na baisikeli zingine zitaenda kwa miradi mbalimbali. UWABA tunashukuru sana Re-cycle kwa mchango huu, na kampuni ya Guta kwa kutusaidia kuingiza nchini. Nunua baisikeli.


Mwenyekiti wa UWABA anashiriki kwenye mkutano wa dunia wa NGOs za Usalama Barabarani

Mwenyekiti wa UWABA anatoa maada kwenye mkutano huko Washington

Mwenyekiti wa UWABA alisafiri huko Washington Merekani kwa Second Global Meeting of NGOs Advocating for Road Safety and Road Victims ulioandaliwa na World Health Organisation tarehe 14-15 Machi 2011. Kwenye mkutano tulifanya mipango kuhusu Decade of Action on Road Safety.

WABATAN - NGO ya wapanda baisikeli wa Tanga - imesajiliwa

UWABA tumesaidia Wapanda Baisikeli Tanga (WABATAN) kupata cheti cha kusajiliwa kama NGO, kwa kufuatilia na ofisi ya usajili wa NGO kwa zaidi ya mwaka. WABATAN imesajiliwa tarehe 6 januari 2011 na namba 21NGO/00004284. Sasa tunafanya mipango kuhusu vipi tunaweza kushirikiana nao kwenye miradi mbalimbali.

Mradi wa re-cycle unanza

Fundi wanapokea vyeti

UWABA wameanza kushirikiana na Re~Cycle NGO huko Uingereza ambayo inawapa baisikeli mashirika hapa Afrika. Kama hatua ya kwanza kwenye ushirikiano, Matt Lawford, fundi baisikeli kutoka Uingereza ambaye anafanya kazi Re~Cycle, amesafiri hapa Tanzania na ametoa mafunzo ya ufundi baisikeli kwa wanachama 15 wa UWABA kwa wiki mbili mwisho desemba 2010 na mwanzo januari 2011.

Tumepata ruzuku kuanzisha Fasta Cycle Messengers

International Centre for Sustainable Cities wametangaza kwamba UWABA tunapewa ruzuku ya kuanzisha Fasta Cycle Messengers Cooperative. Sherehe ya kupokea ruzuku ilitokea tarehe 30 Novemba 2010. UWABA pia tulipata mchango kutoka kwa watu binafsi kwa ajili ya mradi huu. Fedha hizi zitatuwezesha kupata ofisi kwa ajili ya Fasta, kufanya mafunzo, kupata liseni ya TCRA na kutangaza hudumu. Kwa taarifa zaidi na habari za zamani za Fasta angalia hapo chini.

Kampeni ya UNEP ya "Share the Road"

Wawakilishi wa UWABA kwenye mkutano wa Share the Road

Wawakilishi wawili wa UWABA walisafiri huko Nairobi, Kenya kuhudhuria workshop la kampeni ya "Share the Road" ya Afrika Mashiriki tarehe 29 Novemba 2010. "Share the Road" ni kampeni ya United Nations Environmental Programme kuongeza uwekezashi kwenye miundombinu ya watembea kwa miguu na wapanda baisikeli. Mwenyekiti wa UWABA alitoa maada kwenye workshop. Wakati wa kutembelea Nairobi, wanachama wa UWABA pia walisaidia na walishiriki kwenye msafara wa baisikeli ulioandaliwa na Uvumbuzi, NGO ya Kenya, tarehe 28 Novemba. Tunashukuru UNEP na ABN kudhamini UWABA kushiriki kwenye matukio haya.

Siku ya kukumbuka waathirika wa ajali za barabarani

UWABA tulishiriki na mashirika mengine ya usalama barabarani kuandaa na kushiriki kwenye maadhimisho hapa Tanzania kulingana na Siku ya kukumbuka waathirika wa ajali za barabarani tarehe 21 Novemba 2010. Tukio ulitokea huko Mnazi Mmoja Dar es Salaam. UWABA pia tunashirikiana na NGOs zingine zinazohusika na usalama barabarani kuandaa mtandao wa mashirika ya usalama barabarani Tanzania.

Msafara wa Baisikeli 10/10/10

Msafara wa Baisikeli 10/10/10

Wapanda baisikeli 200 walishiriki kwenye msafara wa baisikeli 10/10/10 ulionandaliwa na UWABA pamoja na ForumCC sambamba na siku kuu ya vitendo kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi jumapili tarehe 10/10/10. Baada ya msafara wasanii walioongozwa na Elia Kimena walipiga hip hop kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi na mazingira pamoja na baisikeli, na hotuba zilitolewa na mgeni rasmi Eng. Bonaventure Baya, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na viongozi wengine. Zawadi za baisikeli na helmets zilitolewa kwa bahati nasibu. Tukio hili lilikuwa moja kati ya matukio 7,347 yaliyotokea kwenye nchi 188 duniani kupiga kampeni kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi siku ile ile.

UWABA tunafanya kampeni kuhusu Ilani za Uchaguzi

Mwalimu Nyerere akiendesha baisikeli

Uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Rais wa Tanzania ulitokea mwezi wa Oktoba 2010. UWABA tulifanya kampeni ili vyama vya siasa waweke sera zao kuhusu usalama barabarani na uhamasishaji wa baisikeli kama chombo cha usafiri kwenye Ilani za Uchaguzi. Tumeandika barua kwa vyama mbali mbali vya siasa tangu Januari 2010 na kufuatalia. Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wameweka wazo la njia za baisikeli kwenye barabara kwenye Ilani ya Uchanguzi yao, na vyama vingine wametamka usalama barabarani kwenye ilani zao (hawakutamka kwenye ilani za 2005). Tuliandaa kipeperushi kutoa taarifa kwa wapanda baisikeli kuhusu ilani zinasemaje kuhusu usalama barabarani na wapanda baisikeli.

UWABA tunashiriki kwenye mkutano wa mwaka wa African Bicycle Network

Washiriki kwenye mkutano wa ABN

Tarehe 5-7 Oktoba 2010 mwenyekiti wa UWABA alisafiri Dakar, Senegal kushiriki kwenye mkutano wa mwaka wa Mtandao wa Baisikeli wa Afrika African Bicycle Network, uliotokea sambamba na Congress and Exhibition on African Public Transport ulioandaliwa na African Association of Public Transport na Mkutano wa Expert Group Meeting on “Sustainable Mobility for African Cities – Promoting non-motorized transport options and compact cities as complements to public transport” ulioandaliwa na UN-Habitat. Tunashukuru UN-Habitat na ABN kwa udhamini wa kuhudhuria mikutano hii.

UWABA tunatoa maoni kuhusu barabara ambazo zipo kwenye mipango ya marekebisho

Tarehe 1 Julai 2010 UWABA tulipokea jibu la barua letu kutoka kwa TANROADS yenye mipango ya barabara za Morogoro na Kawawa, na pia barabara ya Kigogo-Ubungo. UWABA pia tuliomba taarifa kutoka kwa JICA kuhusu New Bagamoyo Road (makutano ya barabara ya Morocco mpaka Tegeta) na tulipewa link kwenye website ya JICA . UWABA tumeandika maoni yetu na tunapeleka kwa TANROADS na mashirika mengine. Kwa ujumla, miundombinu ya wapanda baisikeli ni nzuri kwenye michoro ya Barabara za Morogoro / Kawawa, nzuri kwa michoro ya barabara ya Kigogo-Ubungo (lakini bado tuna maoni kuhusu barabara hizi), lakini mbaya sana kwa michoro ya makutano ya Morocco mpaka Tegeta (New Bagamoyo Road). Hapa unaweza kusoma maoni yetu:

Tarehe 17 August 2010 UWABA tulikutana na JICA kuhusu New Bagamoyo Road (Morocco-Tegeta). Tulilalamika kwamba hatukupewa taarifa kuhusu mikutano ya washika dau waliyotamka kwenye ripoti yao. Pia tulisema michoro ni mbaya kwa usalama wa wapanda baisikeli. Tuliomba maoni yetu yatekelezwe. Lakini JICA walisema sasa michoro imekamilika hawawezi kubadilisha wala kutekeleza maoni yetu.

Tarehe 15-16 Septemba UWABA tulihudhuria Joint Infrastructure Sector Review huko Mlimani City Conference Centre. Tulisikiliza ripoti mbali mbali kuhusu miundombinu, tulikutana na watu mbali mbali na tulitoa maoni wakati wa mada kuhusu usafiri wa jiji.

Tarehe 22 Septemba 2010 UWABA tulikutana na TANROADS kuhusu barabara zote tatu na tulipitia maoni yetu pamoja.

Tarehe 24 Septemba 2010 UWABA tulikutana na wataalumu wanaosaidia kuandika upya sera ya taifa ya usafiri (National Transport Policy Review) huko PPF tower kwenye mkutano wa washika dau.

Wiki ya Usalama Barabarani 2010

Wanafunzi wa usalama wa baisikeli, Tanga

UWABA tulishirika kwenye Wiki ya Usalama Barabarani huko Tanga tarehe 9-14 Agosti 2010. Hussein Hamza Hamisi, Hamadi Bwaja na UWABA intern kutoka USA Victora Wilson walisafiri huko Tanga tarehe 4 Agosti. UWABA tulifundisha kozi nzima ya siku mbili kwa wanafunzi wa shule 17 (kutoka Shule ya Msingi Changa, shule ya Msingi Jehudi na Shule ya Msingi Changa Media) na wanachama watatu wa WABATAN tarehe 6-7 Agosti. Washiriki hawa walipewa helmet na reflecter jacket, na pia walipokea vyeti vyao wakati wa uzinduzi wa Wiki wa Usalama Barabarani.

Wakati wa Wiki ya Usalama Barabarani, UWABA tulikuwa na hema kwenye uwanja na tulisambaza taarifa kuhusu usalama wa baisikeli kwa watu waliotembelea. Pia wakati wa wiki, UWABA tulisindikiza traffic police kutembelea shule mbali mbali na tulitoa taarifa kuhusu usalama wa baisikeli (Shule ya Azimio-wanafunzi, Shule ya Mbambani-wanafunzi 26, Shule ya Mwang'ombe-wanafunzi 112, Shule ya Ngamiani Kusini-wanafunzi 63, Shule ya Makorora-wanafunzi 96).

Tunashukuru sana familia na marafiki wa Victoria Wilson kutoa udhamini ili UWABA tushiriki kwenye wiki ya Usalama Barabarani Tanga. Pia tunamshukuru Victoria kwa kazi alizofanya kwa UWABA wakati wa internship.

Wanachama wa UWABA tulibaki Dar es Salaam pia tulishiriki kwenye uzinduzi na ufunguzi wa Wiki ya Usalama Barabarani mkoa wa Dar es Salaam tarehe 9 na tarehe 14 Agosti huko Mnazi Mmoja.

Kuegesha baisikeli Mlimani City

Wapanda baisikeli nje ya Mlimani City

Tarehe 31 Julai 2010 wapanda baisikeli tulikuja pamoja Mlimani City Shopping Centre kulalamika kuhusu sera ya Mlimani city kupiga marufuku wapanda baisikeli kuegesha kwenye maeneo ya maegesho. UWABA tumefuatalia suala hili na Mlimani City tangu 2007 na tunafuatalia jibu la barua zetu lakini mpaka sasa hatupati jibu. Wapanda baisikeli 20 tulienda pamoja Mlimani City pamoja na waandishi wa habari wa Channel 10 news kulalamika na wameneja walikubali kubadilisha sera hii na kuweka sehemu ya kuegesha baisikeli. Baada ya tukio hili wapanda baisikeli wanaenda Mlimani City na sasa tunaruhusiwa kuingia na kuegesha, kwa sababu ya hatua hii tuliyochukua.

UWABA tunashiriki kwenye Velo City 2010 jijini Copenhagen

Filbert Mbecha akiendesha baisikeli huko Copenhagen

Wanachama wawili wa kamati ya UWABA Fredrick (Mejah) Mbuya na Filbert Mbecha, walisafiri huko Copenhagen, Denmark kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa baisikeli jijini Velo City tarehe 22 mpaka 25 Juni 2010. Mwenyekiti wa UWABA Fredrick Mejah Mbuya alitoa maada fupi yenye photos za baisikeli na hali ya miundombinu kwa wapanda baisikeli Dar es Salaam. Aidha UWABA tulichangia mawazo katika mazungumzo, tulikutana na watu wengi wanaohamasisha baisikeli kama chombo cha usafiri jijini na tulishiriki kwenye msafara wa baisikeli Copenhagen. Tunashukuru Velo City outreach program (City of Copenhagen) na UN-Habitat waliofadhili ushirikiano wa UWABA katika mkutano huu muhimu.

Tangazo la redio la Traffic Police

Traffic police wametoa tangazo la redio kuhusu sheria za kuegesha magari. Inasema magari yasiegeshe barabarani na kwenye sehemu inasababisha hatari kwa wapanda baisikeli na watembea kwa miguu.

UWABA tunahudhuria Mkutano wa Barabara za Mkoa wa Dar es Salaam

Tarehe 12 Mei 2010 wanachama wawili wa UWABA tulihudhuria Mkutano wa Barabara za Mkoa wa Dar es Salaam. Mikutano hii hutokea kila baada ya miezi sita na mkutano huu ulikuwa wa kwanza tulialikwa, na rufaa kutoka Meya wa Dar es Salaam. Mkutano ulikuwa mzuri, tulipata taarifa mbali mbali na tulikuwa na nafasi kuchangia mawazo na kuuliza maswali.

Msafara wa Baisikeli 2010

Mbalozi Tim Clarke na Waziri Mhe Margeret Sitta

Msafara wa Baisikeli Dar es Salaam 2010 ulisherekewa na zaidi ya wapanda baisikeli 400, kati wao walemavu 100, zaidi ya misafara yote mengine. Msafara ulikuwa ndani ya Wiki ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Ulaya Tanzania walikuwa wadhamini. Wageni rasmi walikuwa Mhe Margeret Sitta Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto pamoja na Mbalozi Tim Clarke mbalozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania, na wageni waalikwa walikuwa Mbunge Mhe Margreth Mkanga, Bwana Jason Rwiza, Mkurugenzi wa Mipango TANROADS, pamoja na Engineer George Daffa wa TANRAODS, Diwani Leonard Lupilya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Inspector Swai wa Traffic Police na wawakilishi wa polisi na Meya wa Dar es Salaam. Wageni rasmi na wageni waalikwa walishiriki kwa kuendesha baisikeli pamoja na washiriki wengine. Kauli mbiu ilikuwa "Usafiri kwa Wote" chini ya "2010 European Year for Combatting Poverty and Social Exclusion". Baisikeli tano na baisikeli za walemavu 3 zilitolewa kwa washiriki na bahati nasibu. Msafara ulikuwepo kwenye vipindi vya habari vya ITV na Channel 10.

Msafara wa Baisikeli 2010

Hapa unaweza kuona picha zaidi na kupata taarifa zaidi:UWABA tunaanzisha Ushirika wa Fasta Cycle Messengers

"Messengers" au "couriers" za baisikeli wanaonekana sana kwenye majiji ya Ulaya na Merekani - wanapeleka barua na vifurushi kwa haraka mlango hadi mlango jijini. Hapa Dar es Salaam huduma hizi mpaka sasa zinatolewa na magari na piki piki tu na siyo baisikeli. UWABA sasa tunaanzisha ushirika mpya unaoitwa Fasta cycle Messengers Cooperative kutoa huduma hizi za haraka na za kutegemea kwa kutumia baisikeli bila kuchafua hewa za mazingira. Wanachama waanzilishi 16 wa Fasta wametoka wanachama waasisi wa UWABA. Ushirika umesajiliwa tarehe 18 Februari 2010 na sasa tupo kwenye taratibu ya kupata liseni.

Tarehe 10 Aprili 2010 tulifanya "Alley Cat" ya kwanza, imetayarishwa na Adam Mallet, mwanachama mpya kutoka nchi ya Hungary ambaye tayari amefanya kazi kama cycle messenger huko Ulaya. "Alley Cat" ni mashindano na washiriki wanafanya kazi mbali mbali za kibarua kwa baisikeli jijini kwa kushindana, na ni jinsi nzuri kujifunza kuwa messenger mzuri. Hongera kwa Godfrey Jax aliyeshinda Alley Cat, na Sosthenes Amlima na Ally Saidi Mwishehe waliopata nafasi za pili na tatu.

Tarehe 25 Mei 2010 Fasta Cycle Messengers walikuwa na uchaguzi rasmi wa viongozi chini ya usimamizi wa Ofisa ya Ushirika Wilaya ya Kinondoni, Bwana Bukuku. Hongera kwa Hussein Hamza Hamisi aliyechaguliwa kama mwenyekiti, Hamadi Bwaja alichaguliwa kama makamu mwenyekiti, na wanachama wengine wa bodi Godfrey Jax, Kibwana Mohammed, Shamte Kisoma na Mohammed Samwely. Sosthenes Amlima alichaguliwa kama mwakilishi wa wanachama wa kawaida. Filbert Mbecha na Raechel Kayaye walichaguliwa na Bodi kuwa wafanyakazi wa utawala wa Fasta Cycle Messengers.

Kwa sasa tunatafuta michango/ruzuku kutusaidia kuanzisha Fasta Cycle Messengers. Hapa unaweza kusoma muhtasari wa maombi yetu na kwa nini tunahitaji msaada huu:

UWABA tunatoa mawazo kama mshikadau kuhusu Road Regulations

UWABA tumepata nafasi ya kutoa mawazo yetu kuhusu draft regulations chini ya Roads Act. Tarehe 4 Machi, UWABA tulihudhuria mkutano wa washika dau ulioitwa na Wizara ya Miundombinu, na maoni mengi yetu yamekubalikwa. Sasa tunasubiri draft nyingine kutoka wizara.

UWABA tunakutana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam

Tarehe 21 januari 2010 wawakilishi saba wa UWABA tulikutana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe Kimbisa. Tuliongea kuhusu umuhimu wa baisikeli kama chombo cha usafiri jijini na matatizo tunayopata barabarani wakati miundombinu inajengwa bila kuangalia mahitaji yetu. Alisikiliza mawazo wetu na alisema kwamba ni muhimu wapanda baisikeli tuchangie mawazo kwenye sera za barabara. Alitualikwa kwenye mkutano wa mashirika ya serikali na ya siyo ya kiserikali kuhusu barabara utakaotokea mwezi wa tano.

UWABA tunachangia mawazo kwenye barabara za mradi wa TSCP

UWABA tunashirikiana kama washikadau kwenye Transport Sector Consolidation Project (TSCP) chini ya ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI). Mradi huu unahusika maboresho ya barabara za majiji na miji Arusha, Tanga, Kigoma na Mwanza (kampuni ya michoro ni UWP) na Dodoma, Mbeya na Mwanza (kampuni ya michori ni SMEC). UWABA na UWABATAN tumeangalia sana Tanga kuhakikisha kuna usalama barabarani kwa wapanda baisikeli na njia za wapanda baisikeli, na pia tumechangia mawazo kwa ajili ya miji mengine.

Tumefanya mikutano ifuatayo:

Msafara wa baisikeli wa Ride Planet Earth

Washiriki kwenye Ride Planet Earth

UWABA tulifanya msafara wa baisikeli tarehe 6 desemba 2009 mara moja na misafara ya wapanda baisikeli kwenye nchi mbali mbali duniani ili kuita viongozi kupunguza mabadaliko ya tabia ya nchi huko Copenhagen, Denmark, pamoja na kampeni ya Ride Planet Earth. Msafara wetu tulienda Gezaulole kwa Kali Mata. Wanachama wa UWABA pamoja na wanachama wa African Partership on Climate Change Coalition (APCCC).

UWABA tunashiriki kwenye mkutano kuhusu barabara za vijijini Arusha

Watu wanne wa kamati wa UWABA pamoja na mmoja wa UWABATAN tulishiriki kwenye mkutano wa barabara za vijijini ulioandaliwa na Tanzania Roads Association (TARA) pamoja na International Road Federation na Global Transport Knowledge Partnership (gTKP), uliotokea Arusha tarehe 25-27 novemba 2009.

UWABA tunashiriki kwenye siku ya kuwakumbuka waathiriki wa ajali za barabarani

UWABA tulishiriki kwenye kamati kuandaa kwa siku ya kuwakumbuka waathiriki wa ajali za barabarani, na tulishiriki siku yenyewe tarehe 15 novemba 2009. Tulishirikiana na SUMATRA, Chakua, CTS na Amend.

Mikutano ya mabadaliko ya tabia ya nchi

Mkutano wa mabadaliko ya tabia ya nchi, Morogoro

UWABA tunashiriki kwenye mikutano mbali mbali kuhusu mabadaliko ya tabia ya nchi hapa Dar es Salaam na pia huko Morogoro. Tarehe 14 novemba Hussein Hamza Hamisi na Idrisa Zongo wa UWABA walihudhuria mkutano kuhusu mabadaliko ya tabia ya nchi ya Environmental Watch Association of Tanzania (EWAT) Sokoine University of Agriculture (SUA). Walisafiri Morogoro na baisikeli ambayo ni safari ya zaidi ya 200km - walisafiri tarehe 13 na kurudi tarehe 15. Walitoa mada huku kwenye mkutano kuhusu vipi baisikeli ni chombo kinachosaidia kupunguza utoaji wa carbon dioxide.

Jinsi mpya ya kuwasiliana na UWABA


Msafara wa Baisikeli 2009

Sunday News picha ya Msafara wa Baisikeli 2009Msafara wa Baisikeli 2009 ulifanyika tarehe 24 oktoba 2009, na wapanda baisikeli zaidi ya 150 walishiriki. Kaulimbiu ilikuwa mabadaliko ya tabia ya nchi (climate change) na mgeni rasmi wetu alikuwa Mhe Dr. Batilda Burian, Waziri wa Nchi kwenye ofisi ya Makamu Rais anayeshughulika na mambo ya Mazingira. Alitoa hotuba kuhusu shida ya mabadaliko ya tabia ya nchi na vipi wapanda baisikeli tunasaidia kwa kutotoa carbon dioxide. Wadhamini wakuu wetu walikuwa British High Commission (Ubalozi wa Uingereza), na Deputy British High Commissioner, Bwana Tony Brennan, pia alitoa hotuba kuhusu mabadaliko ya tabia ya nchi. Msafara wetu ulikuwa moja katika tukio 5200 kwenye nchi 181 zilizotokea siku ile ile kuamsha dunia kuhusu shida ya mabadaliko ya tabia ya nchi, chini ya kampeni ya www.350.org. Wageni waalikwa Diwani Leondard Lupilya diwani wa Manispaa ya Ilala, Bwana Jason Rwiza Mkurugenzi wa Mipango wa TANROADS, Bi Christine Kayoce mkuu wa usalama barabarani wa TANROADS, na Inspector Abel Baltazar Swai Mlezi wa wapanda baisikeli Traffic Police walishiriki kwa kuendesha baisikeli kwenye msafara na kutoa hotuba kuhusu usalama wa wapanda baisikeli. Kampuni ya Guta walichangia zawadi ya guta na pia tulisambaza zawadi za baisikeli tano, baisikeli ya mlemavu, helmet 20 na reflector jacket 140.

UWABA tunafanya semina pamoja na waalimu wa udereva

Tarehe 6 Oktoba 2009 UWABA tulifanya semina pamoja na waalimu wa udereva kutoka kwa shule za udereva mbali mbali. Tuliongeana kuhusu vipi kuboresha elimu ili kuondoa tatizo la magari kugongana na wapanda baisikeli. Semina hii iliendeshwa chini ya mradi wetu wa Wamba Memorial Fund. Semina ilitokea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Mabibo.UWABA tunashiriki kwenye wiki ya usalama barabarani, Mbeya

Wiki ya usalama barabarani Mbeya

UWABA tulishiriki kwenye wiki ya usalama barabani mkoani Mbeya tarehe 28 Septemba – 3 Oktoba 2009. Tulifundisha kozi ya siku mbili ya usalama wa baisikeli kwa wanafunzi wa shule 20, pamoja na kutoa taarifa kuhusu usalama wa baisikeli.UWABA tunasaidia uanzishaji wa UWABATAN - Umma wa Wapanda Baisikeli Tanga

Mkutano wa kwanza wa UWABATAN

Tarehe 26 Septemba 2009 wapanda baisikeli wa Tanga walianzisha Umma wa Wapanda Baisikeli Tanga (UWABATAN). Wawakilishi wanne wa UWABA Da es Salaam tulisafiri Tanga kuhudhuria mkutano wa kwanza na kusaidia katika uanzishaji.UWABA tunafundisha usalama wa baiskeli shule za Mbondole, Kigamboni na Msongole, na kwa wapanda baisikeli Magomeni

Mafunzo ya usalama wa baisikeli shule ya Kigamboni

UWABA tunaendelea vizuri na mradi wetu wa usalama wa baiskeli, chini ya Wamba Memorial Fund.

Tarehe 27 na 29 Agosti 2009, wanachama sita wa UWABA walifundisha wanafunzi 62 wa sekondari pamoja na watu wazima 3 kwenye shule ya Mbondole, Dar es Salaam. Mgeni rasmi alikuwa Ndugu Kassimu Yusufu Mng’ombe, Diwani wa Kata ya Msongora .

Tarehe 6 na 13 Juni 2009, wanachama wa UWABA ambao wameshahudhuria mafunzo ya wakufunzi, walifundisha wapanda baisikeli wenzao 24 kwa kutumia darasa na uwanja wa shule ya Nyerere, Magomeni. Diwani wa Kata ya Makurumla (Ndugu Rajabu) na Diwani wa Manzese (Ndugu Manumbu) walikuwa wageni rasmi.

Tarehe 21 na 28 Februari 2009, wanachama wanne wa UWABA walifundisha usalama wa baisikeli kwa wanafunzi 37 wa Kigamboni Secondary School, Dar es Salaam. Mama Wamba alikuwa mgeni rasmi.

Tarehe 18 mpaka tarehe 21 Novemba 2008, wanachama sita wa UWABA walifundisha wanafunzi 60 wa sekondari na wanafunzi 55 wa shule ya msingi kwenye shule ya Msongola, Dar es Salaam. Wanafunzi, ambao wanakujaga shuleni na baiskeli, walishirikiana katika mafunzo ya darasa, vitendo na mazungumzo.

UWABA tunakutana na Komanda Kombe, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani

Tarehe 26 agosti 2009, wawakilishi nane wa UWABA walikutana na Komanda Kombe, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, pamoja na ofisa na Inspecta 12 kutoka makau makuu ya Traffic Police. Kwenye mkutano tuliongeana kuhusu matatizo ya magari kuegesha kwenye service roads, kuelimisha wapanda baisikeli kuhusu usalama barabarani na vipi UWABA na traffic police tunaweza kushirikiana vizuri.

Watu wapya kwenye kamati

Hongera Filbert Mbecha na Dominata Rwechungura ambao wamechaguliwa kuwa kwenye kamati ya UWABA jumamosi 22 agosti 2009. Filbert Mbecha ni mweka hazina na Dominata Rwechungura ni mjumbe wa kamati. Juma S Jongo na Rashid Karanji walijitoa kutoka kamati - tunawashukuru kwa kazi nzuri za kujitolea wamezofanya.

UWABA tunashirikiana kwenye Conference ya Usalama Barabarani ya Afrika nzima Dar es Salaam

Wanachama 15 wa UWABA tulishirikiana kwenye Make Roads Safe Africa, 2009 Conference tarehe 8 Julai, na Semina ya Usalama Barabarani tarehe 9 na 10 Julai 2009 hapa Dar es Salaam. Mikutano hii imetayarishwa na Commission for Global Road Safety kama sehemu ya Kampeni ya Make Roads Safe kabla ya Mkutano wa Mawaziri wa Umoja wa Taifa kuhusu Usalama Barabarani huko Moscow mwezi wa Novemba 2009. Makamu Rais wa Tanzania H.E. Dr. Ali Mohamed Shein, alitoa hotuba kwenye conference.

Kwenye mkutano wanachama wa UWABA tulishirikiana kwenye mazungumzo na tulifuatalia kipau mbele kitolewe kwa usalama barabarani kwa watumiaji wa barabara ambao wapo kwenye hatari zaidi na wapanda baisikeli. UWABA pia tulisaini petition ya kuita miaka kumi ya utekelezaji wa usalama barabarani, na tulikutana na Mbalozi wa Kampeni ya Make Roads Safe, Michelle Yeoh.

Wanachama wa UWABA na Mbalozi wa Kampeni ya Make Roads Safe, Michelle Yeoh

UWABA tunashirikiana na NGOs zingine za Afrika kuanzisha African Bicycle Network, huko Nairobi

Mejah Mbuya, Filbert Mbecha na Edgar Paulo wa UWABA walisafiri kwenda Nairobi na kuhudhuria mkutano wa NGOs za Afrika ambao wanashughulika na kuhamasisha wapanda baisikeli tarehe 6 na 7 Julai 2009. Kwenye mkutano huu, African Bicycle Network (ABN) ilianzishwa. Pia tulishirikiana kwenye msafara wa baisikeli uliotayarishwa na shirika la Uvumbuzi.

Wanachama wa UWABA na washiriki wengine kwenye mkutano wa NGOs za baisikeli za Afrika, Nairobi

UWABA tunakutana na JICA

Tarehe 1 Juni 2009, wanachama wa UWABA walikutana na wafanyakazi wa Japanese International Cooperation Agency (JICA). Tuliongeana kuhusu Barabara ya Kilwa, ambayo JICA walidhamini, na Dar es Salaam Transport Master Plan, na vipi mazingira na usalama wa wapanda baisikeli na usafiri wa siyo ya moto unaweza kuboreshwa.

UWABA tunaleta ujumbe wa baisikeli kwenye mkutano Tanga

Tarehe 28 Mei 2009, wanachama wawili wa UWABA walihudhuria mkutano huko Tanga kuhusu "Urban Development and Environmental Management" (maendeleo ya jiji na mazingira), ambapo pia diwani wa halmashauri ya Tanga walihudhuria. Kwenye mkutano huu, UWABA tulichangia mawazo kuhusu vipi uhamasishaji wa baisikeli kama chombo cha usafiri unaweza kufanya jiji lipendeze na liwe jiji la watu siyo jiji la magari. UWABA pia tulimpa Meya wa Tanga, Mhe. Kisauji, helmeti na jaketi ya reflecta.

UWABA tunampa helmeti na reflecta jaketi kwa Mhe Kisauji, Meya wa Tanga

Mwenyekiti wa UWABA anachangia kwenye mkutano wa NGOs za dunia kuhusu usalama barabarani

Tarehe 7-8 Mei 2009, mwenyekiti wa UWABA alihudhuria mkutano wa NGOs wanaofanyakazi katika kuboresha usalama barabarani, huko Brussels, Ubeljiji. Mkutano ulitayarishwa na shirika la afya duniani (World Health Organisation). Alitoa mada kuhusu kazi ya UWABA kuleta usalama barabarani kwa wapanda baisikeli wa Dar es Salaam. Mkutano huu umetengeneza mapendekezo kwenda kwa mkutano wa mawaziri wa usalama barabarani Moscow mwisho wa mwaka huu. UWABA tulisaidia kuhakikisha kwamba mapendekezo kulinda wapanda baisikeli na watembea kwa miguu, na miundombinu inayowalinda, yawe humu.

Mwenyekiti wa UWABA anachangia kwenye mkutano wa ubora wa hewa, Nairobi

Tarehe 21-23 Oktoba 2008, mwenyekiti wa UWABA chairman alihudhuria mkutano wa mradi wa umoja wa taifa wa mazingira (United Nations Environmental Program) kuhusu ubora wa hewa jijini huko Nairobi, Kenya. Kwenye mkutano huu alieleza vipi kuhamasisha baisikeli kama chombo cha usafiri unaweza kusaidia kuboresha ubora wa hewa jijini.

Video kuhusu UWABA, baiskeli na usalama

Mwanachama wa UWABA Amar Shanghavi pamoja na wanachama wengine tumetengeneza video kuhusu UWABA na usalama wa baiskeli.

Msafara wa Baiskeli 2008

Diwani Lupilya Picha ndani ya gazeti ya Sunday Citizen

Msafara wa Baiskeli 2008 ulienda vizuri tarehe 25 oktoba 2008. Wapanda baiskeli 150 walishiriki. Mgeni rasmi Mhe Azzan Zungu mbunge wa Ilala alitoa hotuba kuhusu umuhimu wa baiskeli katika usafiri wa jiji na Diwani Lupilya wa Manispaa wa Ilala aliendesha baiskeli kwenye msafara na aliongea kwenye TV - Channel 10 na DTV. Mbalozi wa Ireland na mume wake waliendesha baiskeli pia. Tulikuwepo ukurasa wa kwanza kwenye Sunday Citizen. Zawadi za baiskeli tatu, baiskeli ya tairi tatu ya abiria, baisikeli ya mlemavu, helmeti 20 na jaketi za reflecta 20 zilitolewa kwa bahati nasibu na walioshinda walifurahi sana. Tunashukuru sana wadhamini wetu Ubalozi wa Ireland na waliochangia huduma/vifaa bure - Kampuni ya guta, Business Times, Manispaa ya Ilala na Ultimate Security. Tunatumaini tumewahi kuonyesha umuhimu wa baiskeli na usalama barabarani kwa wapanda baiskeli Dar es Salaam.Mkutano wa utawala wa sekta ya usafiri, Yaonde, Cameroon

Mejah akitoa maada kwenye mkutano

Tarehe 23-25 Septemba 2008 mwenyekiti wa UWABA, Mejah Mbuya, aliwakilishi UWABA kwenye mkutano wa utalawa wa sekta ya usafiri ya Afrika uliyotokea jiji la Yaonde, Cameroon. Mkutano uliendeshwa na shirika la gTKP. Mejah alitoa maada kuhusu ushirikiano wa UWABA na serekali.

Utafiti kuhusu usafiri wa baiskeli Dar es Salaam

Mwezi wa Septemba 2008 wanachama wa UWABA tumewasaidia watafiti Eyasu Markus Woldesmyas kutoka Ethiopia na Alphonse Nkurunziza kutoka Rwanda ambao wanafanya utafiti kwenye chuo cha ITC, Uholonzi. Utafiti wao ni kuhusu usafiri wa baiskeli Dar es Salaam na UWABA tumesaidia kufanya savei.

Tumehamia

Tarehe 1 Agosti 2008 UWABA tumehamia Manzese Sisi kwa Sisi, baada ya mkataba yetu ya kodi ya ofisi ya zamani ya Mabibo kumaliza. Karibu kutembelea ofisi, ambapo kuna taarifa nyingi kuhusu masuala ya baiskeli ya Dar es Salaam.

Mafunzo ya wakufunzi ya usalama wa baisikeli

Tarehe 21-23 julai 2008 UWABA tuliendesha kozi ya mafunzo ya wakufunzi ya usalama wa baisikeli Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Mabibo. Mwalimu wetu alikuwa bwana Andrew Wheeldon kutoka Bicycling Empowerment Network, Afrika Kusini. Tulipata udhamini kutoka Wamba Memorial Fund kuendesha kozi hii pamoja na mradi wa usalama barabarani kwa wapanda baisikeli tunaoanza sasa. Mafunzo yalikuwa na washiriki 24 - mwakilishi kutoka TANROADS, mwakilishi kutoka Traffic Police, walimu watatu kutoka shule za Msongole na Kigamboni, wawakilishi wawili wa HUWATA na wanachama 14 wa UWABA. Washiriki hawa sasa wanatayarisha kutoa mafunzo haya kwa wanafunzi wa shule mbali mbali mkoa wa Dar es Salaam.

Picha ya wanachama wa UWABA anayetoa alama ya mkono ya kusimama

Uzinduzi wa Ofisi ya UWABA

Tarehe 19 aprili 2008 UWABA tulisherehe uzinduzi wa ofisi wetu. Wawakilishi wa SUMATRA na serekali za mitaa walikuwa wageni rasmi. Aidha tulitoa zawadi za helmeti, t-shirt na jaketi za njano kwa wanachama 27 wanaoshirikiana sana katika chama. Tunashukuru sana IBike / International Bicycle Fund merekani na La Stazione delle Biciclette wa Milan, Italia kwa ajili ya michango kubwa katika utengenezaji wa ofisi na zawadi.

UWABA office opening ceremony

Mkutano na mwakilishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

Tarehe 10 Machi 2008 wawakilishi watano wa UWABA tulikutana na Mama Mlamba, idara ya usafiri Halmashauri ya Jiji ya Dar es Salaam. Hapa unaweza kusoma habari ya mkutano huu:

Semina ya Usalama Barabarani - Chuo cha Taifa cha Usafirishaji

Tarehe 19 januari 2008 Chuo cha Taifa cha Usafirishaji waliendesha semina ya Usalama Barabarani kwa Wapanda baiskeli kwa wanachama 21 wa UWABA.

Washiriki na walimu wa Semina

Washiriki tulifundishwa kuhusu sheria na kanuni za usalama barabarani kwa wapanda baiskeli, alama na michoro ya barabarani na uendeshaji baiskeli kwa kujihami. Mafunzo ya muhimu tuliyopata yalikuwa kuhakikisha baiskeli ipo kwenye hali nzuri, vipi kuendesha baiskeli kwa usalama barabarani, umuhimu wa uheshima kati ya wanaotumia barabara, haki na wajibu wao kama ajali ikitokea, sheria za barabara, makutano ya barabara, mawasiliano barabarani na maana ya alama za barabara.

Mwisho wanachama wa UWABA walishukuru sana Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kwa kutoa hudumu hii nzuri kwa jamii ili kuongeza usalama barabarani kwa wapanda baiskeli. Mkuu wa Idara ya Usalama Barabarani, Bwana Chard Wemba alisema kwamba semina hii ni hatua ya kwanza na Chuo kitapenda kuendelea kushirikiana na UWABA kutoa mafunzo haya kwa wapanda baiskeli wengine.

Mkutano na Idara ya Usalama Barabarani ya Wizara ya Miundombinu

Tarehe 14 januari 2008 wawakilishi wanne wa UWABA tulikutana na Idara ya Usalama Barabarani ya Wizara ya Miundombinu. Kwa bahati mbaya mkutano huu haukuwa na mafanyiko kwa sababu tulipewa dakika 15 tu hata kama tulikuwa na miadi ya saa moja.

Mawasiliano na TANROADS

Mwezi wa kwanza 2008 tumepokea barua ya pili kutoka TANROADS ambayo inajibu maswali yetu ya ziada kuhusu barabara zinazojengwa upya - Barabara ya Sam Nujoma, Barabara ya Nelson Mandela na Barabara ya Kilwa. Jibu hili ilitusaidia na ilijibu maswali mengi. Pia, tulikutana na TANROADS makau makuu tarehe 27 Septemba kutoa mada. Tunaendelea kufuatilia utekelezaji wa mipango.

Hapa unaweza kuangalia jibu:

UWABA tunashirikiana katika Siku ya Uamsho wa Mabadiliko ya Majira

Nje ya ofisi ya Makamu wa Rais Mabadaliko ya majira ni suala muhimu kwa watanazania kwa sababu watanzania wengi wanategemea mvua kwa riziki yao. Wapanda baiskeli wanasaidia katika hiyo shida kwa kutotoa moshi ya carbon dioxide wakati wa kusafiri. Tarehe 8 Desemba 2007 UWABA tulishirikiana na Centre for Energy Environment Science & Technology (CEEST), Envirocare, Joint Environment and Development Management Action (JEMA), Journalists Environmental Association of Tanzania (JET), Legal and Human Rights Centre (LHRC), Tanzania Association of NGOs (TANGO), Tanzania Coalition for Sustainable Development (TCSD), Tanzania Traditional Energy Development and Environmental Organization (TaTEDO) na Tanzania Youth Environment Network (TAYEN) kuandaa msafara wa baiskeli kwa uamsho wa mabadaliko ya majira. Tulisafiri na baiskeli kutoka ofisini kwetu Mabibo mpaka ofisi ya Makamu Rais, ambapo tulitoa hotuba na tulikaribishwa na Kaimu Mkurugenzai Idara ya Mazingira Bwana Stephen Nkondokaya. Hatua kufuata tuliyopanga ilikuwa kusafiri na baiskeli mpaka Ubalozi wa Marekani kuwapa barua kutoka mashirika kumi. Lakini tulisimamishwa na polisi na tuliambiwa hatuwezi kuendelea kama kundi maeneo ya Ubalozi wa Marekani bila barua ya kutualika kutoka Ubalozi wa Marekani. Kabla ya msafara tulikuwa tumeshawapa taarifa kwa polisi na tulikuwa tumeshaomba Ubalozi wa Marekani kutupokea sisi na barua zetu siku ya uamsho wa mabadaliko ya majira, lakini inaonekana kwamba ubalozi hawapo tayari kusikia maoni yetu na hata walisimamisha msafara wetu. Tukio ilionyeshwa kwenye habari ya Channel 10 na katika gazeti la Majira, basi tunatumaini kwamba tulisaidia kutoa ujumbe kuhusu mabadaliko ya majira kwa viongozi wa mataifa wanaokutana jili la Bali, Indonesia.

Bonyeza hapa kupata taarifa zaidi:

Msafara wa Baiskeli Dar es Salaam 2007

UWABA pamoja na CHABADA tulikuwa na Msafara wa baiskeli mzuri tarehe 20 October 2007. Watu zaidi ya 200 walishirikiana katika msafara kutoka Mnazi Mmoja na kuzunguka Dar es Salaam. Wanawume, wanawake, vijana, walemavu na wazima walishirikiana. Mgeni rasmi wetu alikuwa Bwana Leonard Lupilya, diwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Kwenye hotuba tuliongea na tulisikia mambo ya usalama wa wapanda baiskeli, barabara salama kwa wapanda baiskeli na tulihamasisha baiskeli kama chombo kizuri cha usafari jijini. Zawadi za guta, baiskeli tatu, helmeti 20 na jaketi za njano 20 zilisambazwa kwa bahati nasibu kwa washiriki. Tunashukuru wadhamini wetu Ubalozi wa Uholonzi, Kampuni ya Guta, Kampuni ya Bakhresa, Ubalozi wa China, Clouds FM na Manispaa ya Ilala.

Msafara wa baiskeli

UWABA tuna ofisi

Tarehe 9 Augosti 2007 tumepata mchango ya Tsh 400,000 kutoka IBike / International Bicycle Fund na wanachama wetu wamechangia pia kupata ofisi ya UWABA. Ipo Mtaa wa Jitegemee, Mabibo. Kwa sasa tunatengeneza ofisi yetu iwe tayari kuweka taarifa nyingi kuhusu mambo ya baiskeli watu wasome. Pia tumenunua guta ya chama iweze kutupa mapato yakuendelea kukodi ofisi baadaye. Tunashukuru sana michango.

Tumefungua sanduka la posta

Tarehe 13 Augosti 2007 UWABA tumefungua sanduka la posta letu - ni SLP 90361, Dar es Salaam. Tunakaribisha mawasiliano kwa posta.

Mkutano na Carl Bro Associates, consultant ya Nelson Mandela Road

UWABA tulikutana na Carl Bro Associates, kampuni wanaofanya michoro ya Nelson Mandela Road, tarehe 12 julai 2007. Hapa unaweza kusoma dondoo:

Tumefungua akaunti ya benki

Tumefungua akaunti ya benki ya UWABA kwenye National Microfinance Bank tawi ya Magomeni. Namba ya akaunti yetu ni 2052300909.

Sehemu ya mikutano imebadilisha

Tumepata sehemu mpya ya mikutano - Mahakama ya Ndizi, Mabibo, kwa fundi guta karibu na Maktaba Baa. Sehemu hii inafaa sana kwa sababu kuna wapanda baiskeli na wapanda guta wengi katika eneo hili.

Mkutano na Manispaa ya Ilala kuhusu msongamano

Tarehe 15 Mei 2007 UWABA tulihudhuria mkutano wa manispaa wa Ilala kuhusu shida ya msongamano wa magari mjini. Tulitoa mawazo yetu kuhusu vipi baiskeli inaweza kusaidia katika tatizo hili na kuhusu shida kama magari mengi yanayopaki njiani.

Watu wapya kwenye kamati

Hongera Rashid Karanji na Sosthenes Amlima ambao wamechaguliwa kuwa kwenye kamati ya UWABA jumamosi 5 Mei 2007.

Swala la maguta

Wanachama wa UWABA pamoja na waendesha guta soko la Tandale tukisanya watu kusaini barua yetu

Tarehe 4 Aprili 2007 Manispaa ya Ilala walitangaza kwamba maguta hazitaruhusu tena kusafirisha bidhaa katika maeneo ya katikati ya jiji au Kariakoo. Sera hii ingeua biashara za watu wengi, ingeunda matatizo ya kusafirisha bidhaa na ingelete malori kubwa ningi mjini. Picha ya wanachama wa UWABA kwenye gazeti ya Dar Leo

UWABA tumepiga kampeni dhidi ya sera hii. Tumesanya watu 835 kusaini barua yetu inayoenda Manispaa ya Ilala. Tarehe 12 Aprili 2007 tulikutana na Meya wa Ilala kutoa maoni yetu. Tarehe 28 Aprili 2007 Meya ya Ilala ametangaza kwamba maguta na mikokoteni ni ruksa. Tunapongezi Meya kwa utawala bora wa kusikiliza maoni ya watu na kufanya uamuzi mzuri. Tutapenda kuendelea kusaidia Manispaa ya Ilala kurekebisha matatizo ya msongamano jijini.

Mawasiliano na Waziri wa Miundombinu

Tumepata barua kutoka Waziri wa Miundombinu kusema anaunga mkono azma yetu kuunda asasi hii muhimu ya wapanda baiskeli.

Msafara wa baiskeli

UWABA tulishirikiana na AALOCOM na CHABADA kuandaa msafara wa baiskeli tarehe 14 oktoba 2006. Watu wengi walihudhuria na wote wamefurahi. Tulianza Mnazi Mmoja, tukazunguka na tulirudi tena Mnazi Mmoja. Polisi walifunga sehemu ya barabara kwa ajili yetu. Zawadi za baiskeli 5 mpya za California zilitolezwa kwa bahati nasibu. Mstahiki Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dr Mwilima alikuwa mgeni rasmi. Tunatumaini msafara wetu ulihamasisha matumizi ya baiskeli, ulihimiza uendeshaji wa baiskeli, ulizingatia usalama na ulihimiza serikali umuhimu wa kukuweka njia maalum za baiskeli.

Msafara wa baiskeli

Mkutano na TANROADS

Wanachama wa UWABA tulikutana na TANROADS mkoa wa Dar es Salaam tarehe 24 mei 2006. Tulitoa maada ya maoni yetu na tulionyesha picha za barabara tulizopiga. Hapa unaweza kuangalia maada yetu:

Tanzania Social Forum

UWABA tulihudhuria Tanzania Social Forum tarehe 22 mpaka 25 machi 2006 Mnazi Moja. Tumekutana na mashirika mengine na tumewapa watu wengi taarifa kuhusu sisi. Hapa kuna picha ya standi yetu:

UWABA kwenye Tanzania Social Forum

Tumesajiliwa

UWABA tumesajiliwa na Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto chini ya Non-Governmental Organisations Act, 2002. Namba yetu ni 02NGO/0683. Tulisajiliwa tarehe 23 februari 2006 na tulipewa cheti tarehe 2 machi. Pia tumejitambulisha kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam.

Rudi juu

Katiba

Rudi juu

Kamati

Rudi juu

Dondoo za mikutano

Mikutano yote inaendeshwa kwa kiswahili. Dondoo zinapatikana hapa.

Rudi juu

Ripoti za Miaka

Rudi juu

Nunua baisikeli kutoka UWABA!

UWABA tunauza baisikeli ili kupata fedha kuendesha kampeni na miradi zetu. Kawaida baisikeli zinauzwa siku za jumapili kwenye container yetu Kigamboni karibu na "kwa Mwingira". Ukipenda kununua baisikeli tafadhali wasiliane na wakuu wa mradi Godfrey Jax 0717009751 au Hussein Hamza Hamisi 0712182217 na malipo yanaenda (kwa cash, au kwa tigo-pesa au m-pesa au kuingiza kwenye akaunti yetu NMB) kwa mweka hazina wetu Filbert Mbecha 0713849700.

Rudi juu

Taarifa kwa waandishi wa habari, kipeperushi, bango

Gazeti la Sunday Citizen wameshaandika makala kuhusu UWABA tarehe 12 machi 2006. Unaweza kusoma makala hii hapa:

Rudi juu

Matumizi ya baiskeli Dar es Salaam

UWABA tumeshirikiana na Robert Bartlett wa Schorrell Analysis ya Jerumani kutengeneza "The global book of transport - Chapter 2 - Tanzania, bicycles in Dar es Salaam". Unaweza kudownload document hii hapa:

Rudi juu

Mawazo yetu

Tuemandaa orodha zinazifuata:

Rudi juu

Picha

UWABA tunasanya picha za hali za barabara pamoja na matukio yetu:

Sheria na sera za Serikali za barabara na usafiri

Hapa unaweza kusoma sheria za barabara za Tanzania (Kiingereza)

Tumepata baadhi za sheria hizi kutoka tovuti ya Bunge la Tanzania www.bunge.go.tz

Hapa unaweza kusoma sera ya Tanzania ya Usafiri (Kiingereza)

Hapa unaweza kusoma sera za usalama barabarani Tanzania (Kiingereza)

Rudi juu

Takwimu

Mwaka 2008, wapanda baisikeli 516 walikufa kwenye ajali za barabarani Tanzania bara. Idadi ya vifo imeongezekwa sana tangu mwaka 2001 - mwaka 2001 wapanda baisikeli 143 walikufa Tanzania bara. Hii ni sawa na ukuaji kila mwaka 20% kutoka mwaka 2001 mpaka mwaka 2008.

Mwaka 2008, vifo vya wapanda baisikeli 23 vilirekodiwa mkoa wa Dar es Salaam (Ilala-5, Kinondoni-15 na Temeke-3). Idadi ya majeruhi ya wapanda baisikeli mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2008 ilikuwa 364 (Ilala-103, Kinondoni-177 na Temeke-84). 6% ya vifo barabarani mkoa wa Dar es Salaam ni vifo vya wapanda baisikeli (mwaka 2008).

18% ya vifo barabarani Tanzania bara ni vifo vya wapanda baisikeli (mwaka 2008).

Mwaka 2007 mkoa wa Dar es Salaam, kulikuwa na ajali 310 ya wapanda baisikeli. Tanzania bara mwaka 2007, kulikuwa na ajali 1660 ya wapanda baisikeli.

Tanzania bara mwaka 2007, 7% ya vyombo vya usafiri vilivyokuwepo kwenye ajali vilikuwa baisikeli. Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2007, 2% ya vyombo vya usafiri vilivyokuwepo kwenye ajali vilikuwa baisikeli.

Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2007, makosa ya wapanda baisikeli yalisabibisha 2% ya ajali za barabarani. Tanzania bara mwaka 2007, makosa ya wapanda baisikeli yalisabibisha 6% ya ajali za barabarani. Udereva wa hatari ulisababisha 47% ya ajali za barabarani, matatizo ya magari 10%, na mwendo haraka 8%.

Tumepata taarifa hii kutoka Traffic Police Makau Makuu

Rudi juu

Barabara za Dar es Salaam

Hapa kuna ramani ya barabara za Dar es Salaam.

Ramani ya Dar es Salaam

Tumepata ramani hii kutoka tovuti ya TANROADS www.tanroads.org

Rudi juu

Wasiliana nasi

baiskeli ya rangi

Rudi juu